Loading...
Home Michezo Cristiano Ronaldo kanunua kimya kimya gari ya zaidi ya Tsh Bilioni 28

Cristiano Ronaldo kanunua kimya kimya gari ya zaidi ya Tsh Bilioni 28

163
SHARE

Staa wa timu ya taifa ya Ureno na club ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo ameendelea na utamaduni wake wa kupenda kumiliki magari ya kifahari, Ronaldo amekuwa akionekana karibia kila linapotoka toleo la gari jipya na akalipenda basi hatosita kufanya maamuzi ya kulinunua.

Imeripotiwa kuwa Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo ametumia dola milioni 12.4 ambazo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 28 kununua gari aina ya Bugatti La Voiture Noire linalotajwa kuwa ndio gari ghali zaidi Duniani la muda wote, Ronaldo anatajwa kuingiza kipato cha zaidi ya Tsh. Bilioni 78 kwa mwaka.

Bugatti La Voiture Noire toleo la 2019 limezinduliwa rasmi mwezi March 2019, pamoja na kununuliwa na Cristiano Ronaldo na kuwa gumzo mtandaoni, gari hilo ndio linatajwa kuwa lina thamani zaidi kwa sasa duniani na gharama ya gari hilo unaweza kununua Private Jet.

Facebook Comments