Loading...
Home Michezo SIMBA AU YANGA KUKIPIGA NA SEVILLA YA HISPANIA JIJINI DAR

SIMBA AU YANGA KUKIPIGA NA SEVILLA YA HISPANIA JIJINI DAR

68
SHARE

DODOMA, 
Tanzania -Mabingwa mara moja  na mabingwa mara tano wa UEFA Europa League, Sevilla FC wanatajariwa kutua nchini Tanzania kwa ziara ya kihistoria ya kimichezo inayodhaminiwa na kampuni ya SportPesa kwa kushirikiana na Uongozi wa Ligi Kuu nchini Hispania, La Liga inayokwenda kwa jina la ‘LaLiga World’
Sevilla ambayo ni klabu ya kwanza kutoka nchini Hispania kuzuru nchini Tanzania, itacheza mechi ya kirafiki na moja kati ya vilabu vya Simba au Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Mei 23.

Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema ziara hiyo ni muendelezo wa ahadi ya kampuni hiyo ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.

“SportPesa inapenda kuendelea kushirkiana na La Liga ambayo inatajwa kuwa Ligi bora duniania ili kuvinadi vipaji vilivyopo nchini pamoja na kukuza kiwango cha soka nchini
Wakiwa nchini Tanzania, Sevilla ambao wanagombea nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao, watashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

Muendelezo wa historia
“Mwaka 2017 dunia ilishuhudia klabu ya Everton ikitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza na muitikio ulikuwa ni wa kipekee. Hivyo tukaona umuhimu wa kuendeleza historia hiyo kupitia ushirika na LaLiga “Kutokana na kuwa na ushirika na taasisi kubwa za soka duniani, tukaona basi ni vyema kuendeleza kuleta msisimko wa soka nchini Tanzania wenye hadhi sawa na ule wa Everton kwa kuileta timu ya Sevilla nchini Tanzania ambayo ni moja ya vilabu bora barani Ulaya kwa kushirikiana na wenzetu wa LaLiga,” alisema Ndugu Tarimba “Lengo ni kuionesha dunia kuwa Tanzania ni mahala sahihi kwa vilabu vikubwa duniani kuja kwa ajili ya ziara za maandalizi ya Ligi bila kusahau kuvinadi vipaji adhimu vya soka vilivyosheheni nchini”. Uzoefu wa Kimataifa
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya LaLiga Kimataifa, Ndugu Óscar Mayo amesema  kuwa ziara hii itaitangaza Tanzania kimataifa na kufungua milango kwa fursa nyingi zenye kubadili Maisha

Facebook Comments