Loading...
Home Michezo JUVENTUS: CRISTIANO RONALDO, ATACHEZA DHIDI YA AJAX

JUVENTUS: CRISTIANO RONALDO, ATACHEZA DHIDI YA AJAX

111
SHARE

KOCHA wa Juventus, Massimiliano Allegri, amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba supastaa wake, Cristiano Ronaldo, atacheza dhidi ya Ajax kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Aprili 10.

Ronaldo, 34, alipata majeraha ya paja akiwa katika majukumu ya timu ya taifa wiki moja iliyopita, na ameshakosa michezo minne mfululizo ya Juventus.

“Cristiano Ronaldo anapambana kurejea, tunatarajia kuwa naye kwa ajili ya mchezo wa Ajax,” alisema Allegri.

Anapambana vizuri na ni lazima tuwe na matarajio kila siku.

“Mguu wake unaimarika na bado kuna siku nane (tangu juzi) kabla hatujacheza jijini Amsterdam, kwa hiyo tuna muda wa kutathmini.

Tunatakiwa kuwa makini na kila kitu.” Hat trick ya Ronaldo ndiyo iliyoisaidia Juventus kutinga robo fainali baada ya kupindua matokeo ya kufungwa 2-0 dhidi ya Atletico Madrid.

Facebook Comments