Loading...
Home Habari Kutana na familia inayotemebea kwa kutumia miguu na mikono (+video)

Kutana na familia inayotemebea kwa kutumia miguu na mikono (+video)

133
SHARE

Hii ni Familia inayopatikana nchini Uturuki ambayo hutembea kwa kutumia miguu na mikono kwa pamoja tofauti na Watu wengine, Wanasayansi wanadai Familia hii inasumbuliwa na tatizo linalowafanya wakose balansi wakitembea kwa miguu peke yake hivyo kuwalazimu kutumia na mikono.

Inaelezwa kuwa familia hiyo ina Watoto watano wenye tatizo hilo na iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005  na cha kushangaza zaidi ni kwamba Wazazi wa Watoto hao hawana kabisa tatizo hilo hivyo wao hutembea kawaida kama Binadamu wengine.

Wanasayansi wanasema tatizo hilo hushambulia sehemu ya ubongo inayohimili balansi hivyo kuwafanya kukosa balansi ya kutembea kwa miguu peke yake.Aidha bado haijajulikana tiba ya tatizo hilo la kimwili ambalo sio la kawaida.

Facebook Comments