Loading...
Home Habari Mahakama mkoani Mwanza yawahukumu wafanyabiashara wa madini

Mahakama mkoani Mwanza yawahukumu wafanyabiashara wa madini

67
SHARE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Mwanza imewahukumu kwa pamoja wafanyabiashara wanne wa madini Jijini Mwanza kifungo cha miaka 38 jela ama kulipa faini shilingi milioni 529.8 baada ya kukiri makosa tisa yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo uhujumu uchumi, rushwa na utakatishaji fedha.
Watuhumiwa wengine wanane ambao walikuwa askari polisi wamerudishwa rumande hadi Aprili 10, 2019 baada ya kukana mashtaka yanayowakabili. Waliohukumiwa ni Said Abdalla, Kisavu Nkinda, Emmanuel Kija na Hassan Sadick.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa Mwanza, Mhe. Rhoda Ngimilanga. Washtakiwa walikamatwa Januari 04,2019 wakituhumiwa kutorosha shehena ya madini ya dhahau, kukutwa na mamilioni ya fedha huku askari wakidaiwa kupewa rushwa ili kuwasindikiza.

Facebook Comments