Loading...
Home Michezo TANZANIA OYEEE, TAIFA STARS YAIGONGA UGANDA 3-0 NA KUFUZU AFCON 2019

TANZANIA OYEEE, TAIFA STARS YAIGONGA UGANDA 3-0 NA KUFUZU AFCON 2019

167
SHARE

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kuvuka kihunzi cha mwisho katika Uwanja wa Taifa na kufuzu michuano ya mataifa Africa AFCON. 
Taifa Stars imeibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ‘ The Cranes’, bao la kwanza likifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 21, Erasto Nyoni dakika ya 51 na Aggrey Morris akimalizia bao la tatu katika dakika ya 57 na kupelekea Tanzania kutimiza ndoto yake ya muda mrefu kushiriki michuano hiyo.
Kwa ushindi huo Taifa Stars inafuzu fainalim za AFCON nchini Misri ikiwa katika nafasi ya pili kwenye kundi L, kwa jumla ya pointi 8, Lesotho ikishuka hadi nafasi ya tatu kwa pointi 6 baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Cape Verde ambayo imemaliza mkiani kwa pointi 5.
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Tanzania kushiriki michuano ya AFCON ni mwaka 1980 nchini Nigeria, ambapo sasa baada ya kufuzu michuano hiyo, inaungana na Uganda, Kenya na Burundi kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki.

Facebook Comments