Loading...
Home Habari Lowassa Aishukuru CHADEMA….Ataka Waliompigia Kura Wamuunge Mkono Rais Magufuli

Lowassa Aishukuru CHADEMA….Ataka Waliompigia Kura Wamuunge Mkono Rais Magufuli

311
SHARE

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amekishukuru Chama cha Demokrasia na Maendeleo, huku akiwaomba wafuasi wa chama hicho wasimuwekee maneno mdomoni.

Akizungumza leo Monduli, Jijini Arusha kwa mara ya kwanza tangu aliporejea ndani ya Chama Cha Mapinduzi wiki mbili zilizopita amesema amerudi CCM kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli na kasi.

“Nimerudi CCM kwa kuwa nimeshawishiwa na Kazi nzuri inayofanywa na Rais pamoja na mawaziri wake nchi nzima. Nimekuja kuwaombeni tumuunge mkono. Kwa CHADEMA nawashukuruni sana. Msiniwekee maneno mdomoni.”

Edward Lowassa leo amewasili nyumbani kwake Monduli Arusha kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza kujiondoa kama Mwanachama wa CHADEMA, chama alichojiunga nacho 2015 ambapo alikuwa mgombea wa kiti cha uraisi.

“Kwenye uchaguzi nilipata kura zaidi ya milioni sita si haba, naomba wote walionipigia kura tumuunge mkono Rais John Magufuli.”-Lowassa

Mwanasiasa huyo Mkongwe nchini Tanzania, Edward Lowassa, mnamo mwaka 2015 alitangaza kujiengua ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA huku akiipeperusha Bendera ya  Chama hicho katika nafasi ya Urais na kushindwa na Mpinzani wake Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Facebook Comments