Loading...
Home Michezo Unai Emery kamwambia Ozil yuko huru kuondoka

Unai Emery kamwambia Ozil yuko huru kuondoka

107
SHARE

Habari kubwa kwa sasa katika usajili wa dirisha dogo barani Ulaya ni pamoja na hii ya kiungo wa Arsenal Mesut Ozil kudaiwa kuwa yupo katika wakati mgumu chini ya kocha Unai Emery ambaye imeripotiwa na BBC 5 Radio Live kuwa kuna tetesi kutokea Arsenal zinaeleza kuwa Unai amemruhusu Ozil kuondoka.

Inadaiwa kuwa Ozil ambaye analipwa mshahara wa pound 350000 kwa wiki ndani ya Arsenal, amekuwa hayupo katika mipango ya kocha Unai Emery, hivyo amempa uhuru mchezaji huyo wa kutafuta timu katika dirisha hili dogo la mwezi January.

Mtangazaji wa BBC Live Radio David Ornstein ameeleza kuwa Ozil hana nafasi tena licha ya yeye mwenye kutokuwa na mpango wa kuondoka timu hiyo mwezi January ” Unai amependekeza Ozil kuondoka Arsenal hilo ndio litakuwa jambo bora kwake na club pia inaonesha kama ingependa Ozil aondoke”

Facebook Comments