Loading...
Home Michezo Ronaldo katwaa taji la kwanza na kuiweka Juventus kwenye rekodi mpya

Ronaldo katwaa taji la kwanza na kuiweka Juventus kwenye rekodi mpya

135
SHARE

Cristiano Ronaldo akiwa ametua club yake mpya ya Juventus kwa mara ya kwanza, anafanikiwa kutwaa taji lake la kwanza akiwa na Juventus kwa mafanikio, baada ya kuisaidia kuifungia goli pekee kwa kichwa dakika ya 61 dhidi ya AC Milan katika ushindi wa goli 1-0.

Ronaldo anaisaidia Juventus kutwaa taji la Super Cup nchini Italia likiwa ndio taji lake la kwanza toka ajiunge na timu hiyo mwanzoni mwa msimu wa 2018/2019 lakini hilo linakuwa ni taji la nane la Super Cup kwa Juventus kutwaa baada ya kutwaa kwa mara ya kwanza mwaka 1995.

Hata hivyo goli la Ronaldo linamaliza ukame wa miaka minne wa taji hilo, mara ya mwisho Juventus kutwaa taji hilo ilikuwa mwaka 2015, hivyo wanaweka rekodi ya kuwa club pekee kuwahi kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi, ikiwa leo wametwaa taji hilo kwa mara ya nane katika historia (1995, 1997, 2002, 2003, 2012, 2013, 2015 na sasa 2019).

V

Facebook Comments