Loading...
Home Michezo Hizi ndio game 7 atazozikosa Harry Kane wa Tottenham

Hizi ndio game 7 atazozikosa Harry Kane wa Tottenham

108
SHARE

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya England Harry Kane ameripotiwa kuwa jeraha lake la kifundo cha mguu alilolipata katika game dhidi ya Man United, litamuweka nje ya uwanja hadi mwezi March na kupelekea kukosa game saba za timu yake.

Harry Kane aliumia dakika za lala salama wakati wa mchezo dhidi ya Man United uliomalizika kwa Tottenham kupokea kichapo cha goli 1-0, pasi nzuri ya Paul Pogba kwa Marcus Rashford dakika ya 44 ndio iliyoimaliza Tottenham na kuiacha iishie kuongoza kwa hali ya umiliki wa mpira na kupoteza point tatu nyumbani.

Baada ya uchungunzi kufanyika kutokana na jeraha la Kane na kusemekana atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi ni atakosa game muhimu ya nusu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Chelsea January 24 na mchezo wa Champions League dhidi ya Borussia Dortmund February 13 na game zingine atazozikosa ni Crystal Palace, Fulham, Watford, Newcastle na Leicester City.

Facebook Comments