Loading...
Home Habari RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI..ATEUA MAKATIBU

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI..ATEUA MAKATIBU

112
SHARE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuteua Mawaziri, Makatibu wakuu na Balozi, ambapo miongoni mwa watu walioteuliwa ni daktari aliyeongoza timu ya matabibu kumuokoa Tundu Lissu alipopigwa Risasi mwaka 2017.

Dkt. Mpoki Ulisubisya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, ameteuliwa kuwa Balozi ambaye Ubalozi wake bado haujatangazwa, na ndiye aliyeongoza timu ya madaktari kumuokoa Tundu Lissu mkoani Dodoma.
Uteuzi huo ambao umetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, pia Rais Magufuli amemteua Bi. Angela Kairuki kuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu / Uwekezaji, na kumpandisha cheo Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kuwa Waziri wa Madini, na Naibu wa pili wa wizara hiyo Stanslaus Nyongo kuendelea kuwa Naibu Waziri.
Pia Rais Magufuli ameteua Makatibu Wakuu wanne, na Naibu Makatibu Wakuu wawili, ili kujaza nafasi za Makatibu Wakuu waliostaafu.
TAZAMA ORODHA KAMILI HAPA CHINI:
Angela Kairuki – Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/UwekezajiDotto Biteko – Waziri wa MadiniStanslaus Nyongo – Naibu Waziri Madini
Joseph Nyamhanga – Katibu Mkuu TAMISEMI
Zainabu Chaula – Katibu Mkuu Afya
Elius Mwakalinga – Katibu Mkuu Ujenzi
Doroth Mwaluko – Katibu Mkuu Sera
Doroth Gwajima – Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Francis K Michael – Naibu Katibu Mkuu UTUMISHI
Sambamba na hayo yote Rais Magufuli amefungua Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba ambao utakuwa katika mji wa Havana, na Balozi wake atatangazwa hivi karibuni.

Kuwa Mjanja

Facebook Comments