Loading...
Home Burudani na Wasanii Sakata la unyanyasaji wa kingono, R Kelly bado hali tete (+videos)

Sakata la unyanyasaji wa kingono, R Kelly bado hali tete (+videos)

189
SHARE

Baada ya jina la  Muimbaji mkongwe kutokea Marekani R Kelly kushika headlines kutokana na kupamba moto kwa sakata lake la unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wenye umri mdogo, mtandao wa Spotify ulitangaza kuongezeka kwa mauzo yake ya muziki hadi kufikia asilimia 16 baada ya kipande cha filamu ya ‘SurvivingRKelly’kuonyeshwa.

 January 05,2019 mtandao wa TMZ umeripoti kuwa R Kelly ameonekana kutofurahishwa na vipande vya filamu hiyo ambavyo vimegusa kwa undani zaidi kuhusu tuhuma zake za unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo ambao baadhi ya wasichana hao wameonekana kutoa ushahidi wa unyanyasaji waliofanyiwa.

Kwa upande wa R Kelly amesema kuwa baadhi ya wasichana hao hawafahamu na wengi wanamchukia kwa matatizo yao binafsi pia ameeleza kuwa kuna watu walitaka kukaa kwenye camera kumtetea lakini watayarishaji wa filamu hiyo walikataa.

Filamu hiyo imewagusa watu wengi maarufu duniani ambapo rapper Chance The Rapperametoa taarifa kuwa anajutia kuwahi kufanya kazi na R Kelly, pia mke wa zamani wa R Kelly amabye ni Andrea Kelly ametoa ushuhuda wa kufanyiwa vitendo hivyo.

Facebook Comments