Loading...
Home Burudani na Wasanii MASTAA WALIOCHANGIA WAPENZI

MASTAA WALIOCHANGIA WAPENZI

293
SHARE

Mario Balotelli na Neguesha.

MKWANJA mwingi kwenye walleti, nyumba kali, maisha freshi, usafi ri mkali, umaarufu ndivyo vinavyosababisha wanawake wengi kuvutika kuwa kimapenzi na wacheza soka wakiamini vitu hivyo kwao haviwapigi chenga.

Wala siyo sapraizi hii na imekuwa kawaida katika ulimwengu wa sasa kwani hata wanawake na wenyewe wamekuwa wakijaribu kuweka mbinu mbalimbali ili kuwanasa wanasoka maarufu duniani.

Neguesha.

Kutokana na hilo, wachezaji wengi wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano mwingi na wakati mwingine wamekuwa wakichanganyana wapenzi na wanandinga wenzao. Hapa chini ni baadhi ya mastaa waliojikuta wakichangia wanawake kwa wakati tofauti.

Aida Yespica na Ozil

SERGIO RAMOS / ALEXIS RUANO / SERGIO SANCHEZ: ELISABETH REYES

Elisabeth Reyes ni modo pia ni alikuwa Miss Hispania mwaka 2006. Alianza kuwa kwenye uhusiano na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos ambapo alidumu naye kwa mwaka mmoja kisha wakaachana. B a a d a ya hapo mrembo h u y o akatua kwa beki Alexis Ruano ambaye wakati huo alikuwa akicheza Getafe na sasa yupo Al Ahli ya Saudi Arabia, hata hivyo hakudumu sana baadaye akazama tena kwa mchezaji mwingine, Sergio Sanchez ambaye anakipiga Cadiz. Kwa sasa wameoana na wamejaaliwa kupata mtoto mmoja.

Nasri na Anara.

MESUT OZIL / MATTEO FERRARI: AIDA YESPICA

Unaambiwa Ozil alivyonasa tu kwenye penzi za huyu Aida ambaye alikuwa Miss Venezuela mwaka 2002 utendaji kazi wake pale Real Madrid ulipungua, mapenzi yakamteka sana na safari za kwenda Italia mara kwa mara kumuona mpenzi wake huyo zilikuwa hazikatiki baada ya hapo mshambuliaji huyo akauzwa Arsenal.

Baadaye wawili hao waliachana na miaka miwili mbele, Aida akiingia kwenye uhusiano na beki wa zamani wa Montreal Impact, Matteo Ferrari ambaye amezaa naye mtoto mmoja.

CRISTIANO RONALDO / SERGIO RAMOS: NEREIDA GALLARDO

Beki wa Real Madrid, Ramos alionekana kudatishwa na muonekano wa Nereida Gallardo mara tu baada ya kukutana naye kwenye klabu ya usiku pale Madrid mwaka 2007, wakiingia kwenye uhusiano. Baadaye mrembo huyo aliweka wazi kuwa pia alikutana na Ronaldo kwenye klabu ya usiku huko Mallorca mwaka 2008.

Wakaingia kwenye uhusiano kwa miezi kadhaa kisha wakatemana huku picha zao wakiwa wanakula bata zikibaki mtandaoni.

MARIO BALOTELLI / CHEIKHOU KOUYATE / MARIO LEMINA: FANNY NEGUESHA

Balotelli na Neguesha walichumbiana kabla ya Kombe la Dunia 2014. Hata hivyo wawili hao waliachana miezi michache baadaye. Baada ya upweke sana, zikaibuka kwamba Fanny anatoka kimapenzi na kiungo wa Crystal Palace, Cheikhou Kouyate baada ya kutupia picha zao mtandaoni.

Kwa sasa Fanny yupo kwenye uhusiano na staa wa Southampton, Mario Lemina ‘playboy’ ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume mwaka jana.

Lemina na Neguesha.

KEVIN-PRINCE BOATENG / CHRISTIAN VIERI: MELISSA SATTA

Mlimbwende Satta alianza uhusiano na mshambuliaji wa zamani wa Inter na Milan, Christian Vieri kati ya mwaka 2006 na 2011 baada ya hapo wakaachana. Mtangazaji huyo wa runinga, alitimba hadi kwa mchezaji aliyeshindwa kuonyesha uwezo kwenye Premier league, Kevin-Prince Boateng ambaye kwa sasa anacheza Sassuolo, mpaka sasa wapo pamoja na wana mtoto mmoja wa kiume.

CRISTIANO RONALDO / MARIO BALOTELLI: RAFFAELLA FICO

Modo Fico inaaminika alitoka na Cristiano Ronaldo mwaka 2009. Hata hivyo baada ya kuachana na Ronaldo aliangukia kwenye penzi la Mario Balotelli ambaye wakati huo alikuwa akicheza Manchester City mwaka 2011 hata hivyo baadaye waliachana. Hata hivyo, Fico aliwahi kutangaza kuwa alikuwa na ujauzito wa Balotelli. Mshambuliaji huyo alikataa na wakalazimika kufanya vipimo ili kubaini kama kweli au la ‘DNA’ ndipo ikaonekana Fico alikuwa sahihi.

Ronaldo na Neledana

SAMIR NASRI / FREDDIE LJUNGBERG / KEIRAN RICHARDSON / DARREN

BENT / JERMAINE PENNANT: ANARA ATANES

Huyu mwanamke anapenda sana wanasoka! Muigizaji Anara alikuwa kwenye uhusiano na nyota wa zamani wa Arsenal, huku pembeni akichepuka na Keiran Richardson.

Ishu hii ilibumburuka baada ya Anara kuonekana na Richardson wakipata chakula cha usiku kisha kwenye Klabu ya Manchester United.

Pia amewahi kuhusishwa kutoka na mastaa wengine kama Darren Bent na Jermaine Pennant na nyota wa mwisho kutajwa kuwa naye ni Samir Nasri.

Facebook Comments