Loading...
Home Burudani na Wasanii UJUMBE WA BASATA KWA DIAMOND ALICHOKIFANYA SUMBAWANGA

UJUMBE WA BASATA KWA DIAMOND ALICHOKIFANYA SUMBAWANGA

1012
SHARE

Baraza la sanaa Taifa (BASATA) limechukua uamuzi wa kumpongeza msanii wa muziki nchini Tanzania Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kuonyesha moyo wake wa kujitolea. Baraza hilo limetumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe kwa msanii Diamond na kuchukua nafasi hiyo kuwaomba wasanii wengine kuiga mfano wake wa kuisaidia jamii inayowazunguka.

Basata wameandika katika ukurasa wao wa Instagram, “Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), linampongeza msanii Nasibu Abdul maarufu kama ‘Diamond Platnumz’ kwa moyo wa kizalendo aliouonesha wa kujitolea shilingi milioni 68 kumalizia ujenzi wa shule iliyopo Wilayani Sumbawanga.

Kitendo hiki kinazidi kuishawishi jamii kuithamini, kuilinda na kuipenda sanaa yetu nchini. Aidha Baraza linapenda kutumia nafasi hii kuwasihi wasanii wengine nchini kuiga moyo huu ili tuweze kuisaidia jamii yetu inayotuzunguka. SANAA NI KAZI, TUIPENDE NA KUITHAMINI.#HongeraDiamondPlatnumz

Facebook Comments