Loading...
Home Michezo Shabiki wa Messi atoroka baada ya familia yake kupokea vitisho kutoka kwa...

Shabiki wa Messi atoroka baada ya familia yake kupokea vitisho kutoka kwa Taliban

124
SHARE

Kijana mdogo wa Afghanistan aliyepata umaarufu mitandaoni kutokana na ushabiki wake sugu kwa mchezaji nyota wa kutoka Argentina Lionel Messi amelazimika kutoroka nyumbani.

Murtaza Ahmadi ambaye sasa ana mika saba alipata umaarufu mwaka 2016 baada ya kupigwa picha akiwa amevalia mfuko wa plastiki unaofanana na jezi ya Messi.

Baadae alikutana na nyota huyo nchini Qatar.

Familia yake imelazimika kutoroka nyumbani baada ya kupokea vitisho kutoka kwa kundi lenye itikadi kali la Taliban.

Walikuwa wakiishi kusini mashariki mwa mkoa wa Ghazni – ambao umekuwa ukilengwa na wanamgambo wa Talin – sasa wamekimbilia mji mkuu wa Kabul.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP familia hiyo ilijaribu kutoroka mwaka 2016 lakini ikarejea tena mkoani humo baada ya kuishiwa na pesa za matumizi.

Murtaza alikuwa na miaka mitano wakati alipovalia tishet ya mfuko wa plastiki uliyo na ransi ya bendera ya ya timu ya taifa ya Argrntina ambayo nahodha wake ni Messi

Baada ya picha hiyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii watu walitoa wito wa kumuomba Messi kukutana nae,wito ambao nyota huyo aliuitikia.

Jina la mvulana huyo lilipotolewa mchezaji huyo alimtumia zawadi ikiwemo shati iliyopigwa saini kupitia shirika la umoja wa Mataifa ambalo anafanyia kazi kama balozi mwema.

Murtaza baadae alialikwa kukutana na Messi wakati nyota huyo wa Barcelona alipozuru Doha kwa mechi ya kirafiki mwaka 2016.

Kijana huyo mdogo aliondoka uwanjani na nyota wake wa kandanda anayemuenzi duniani.

Hata hivyo familia yake inahofia umaarufu aliyopata kutokana na tukio hilo umemfanya kulengwa na wanamgambo wa Taliban.

Mama yake Shafiqa, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa baadhi ya watu wanampigia simu wakisema, ‘Umekuwa tajiri, tupatie pesa ulizopokea kutoka kwa Messi la sivyo tutamteka mtoto wako”

Anasema hawakuweza kitu chochote kutoka nyumbani ikiwa ni pamoja wa shati mwanawe aliyopewa na Messi.

Walilazimika kutoroka usiku wa manane walipoanza kusikia milio ya risasi.

Eneo la Ghazni liko chini ya ulinzi wa serikali lakini lanatajwa kuwa kiungo muhimu katika mzozo kati ya serkali ya Afghanistan na wanamgambo wa Taliban.

Kundi hilo la kislam lenye itikadi kali lilishambulia eneo hilo mwezi Agosti na kuimarisha upya mashambulio hayo mwezi Novemba katika hatua ambayo imewafanya maelfu ya watu kutoroka makwao.

Mamia ya raia wa Afghanistan miongoni mwao – maafisa wa kijeshi na wapiganaji hao wameuawa tangu ghasia zilipozuka.

Ndugu wa kiume wa Murtaza mwenye umri wa miaka 17, Humayoon, ameiliambia shirika la habari la Efe kuwa ameshindwa kumpeleka shule kwa miaka miwili sna kwamba hawamruhusu kucheza nje na watoto wenzake.

“Namkosa Messi,”Murtaza alisema alipokutana na mwandishi wa AFP mjini Kabul. Amesema kuwa anatajia kukutana tena na messi kwa mara nyingine tena.

“Nikimuona nita msalimia ‘Salaam’ na kumuuliza ‘Vipi hali yako?’ Najua atanijibu na kuniambia asante, na baada ya hapo nitaenda uwanjani na [amoja nae ambapo atacheza mimi nikimtizama.”

Facebook Comments