Loading...
Home Michezo Samatta kaungana na Gareth Bale kumnyanyasa Karius

Samatta kaungana na Gareth Bale kumnyanyasa Karius

206
SHARE

Leo tena Karius akiichezea Besiktas ya Uturuki katika game ya UEFA Europa Leaguedhidi ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana SambattaKariusamekutana tena na umahiri na ufundi wa Samatta.

 

Samatta katika game ya tatu ya Europa leo ameisadia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi wa magoli 4-2, Mbwana Samatta akihusika katika upatikanaji wa magoli matatu kati ya hayo akifunga magoli mawili dakika ya 23 na 70 na kutoa pasi ya goli.

Goli la tatu la KRC Genk lilifungwa na Ndongala dakika ya 81 la nne na Piotrowskidakika ya 83 wakati magoli pekee ya Besiktas yalifungwa na Vagnar Love dakika ya 74 na 86, ushindi huo sasa unaifanya Genk kuongoza Kundi I kwa kuwa na point sita wakipoteza mchezo mmoja nafasi ya pili ikifuatiwa na Sarsborg 08 wenye point nne.

Samatta anazidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tuzo ya ufungaji bora wa michuano hiyo, kwani amefunga jumla ya magoli matatu hatua ya makundi akiwa na wastani wa kufunga goli moja kila mechi lakini katika list ya wanaoongoza kwa ufungaji magoli mengi yupo nafasi ya pili akifungana na wachezaji wengine wanne, Munas Dabbur wa RB Salzburg akiongoza kwa kuwa na magoli matano.

 Katika michuano ya Europa League Samatta msimu huu kuanzia hatua ya Makundi hadi game za mwanzo za Play off amecheza jumla ya game nane, tatu za makundi na tano za Play off akifunga jumla ya magoli 9 na  kutoa assist 2 mbili pekee.

Facebook Comments