Loading...
Home Burudani na Wasanii Meneja Afungukia ‘U-Freemason’ Wa Davido

Meneja Afungukia ‘U-Freemason’ Wa Davido

187
SHARE

MENEJA wa staa wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, Asa Asika amekanusha tetesi zilizoenea wiki iliyopita dhidi ya Davido kuwa ni mmoja kati ya watu wanaoabudu katika madhehebu ya siri yaani ‘Freemason’ baada ya Tobi Adegoke ambaye alishawishiwa kujiunga katika Kundi la Black Axe Cult kwa ahadi kuwa itakuwa rahisi kwake kuonana na Davido.

Kijana huyo ambaye alikamatwa wiki iliyopita na hadi sasa yupo kituo cha polisi cha Lagos nchini humo alisema alidanganyika na watu waliomuambia kuwa akijiunga huko itakuwa rahisi kuonana na Davido na akishaonana naye itamsaidia ‘kumboost’ katika muziki wake.

“Mimi ni mshirika wa Black Axe, nimekuwa katika kundi hili kwa muda wa miaka miwili niliambiwa kuwa Davido ni mshirika pia wa kundi hilo kwa hiyo nijiunge ili nikutane naye na itakuwa rahisi kwake kunisaidia katika muziki wangu mwisho wa siku nitakuwa maarufu.

“Pia huyo mtu ambaye alinishawishi nijiunge aliniambia yeye anamfanyia kazi Davido kwa hiyo itakuwa rahisi yeye kuniunganisha naye lakini tangu nimejiunga sijawahi kukutana na Davido,” aliongea huku akilia.

Baada ya kuenea kwa habari hizo, alitafutwa Davido lakini hakupatikana kwa sababu yupo Marekani ‘anashow’ ila walifanikiwa kumpata meneja wake, Asa Asika ambaye naye alifunguka haya;

“Hayo madai kuhusu Davido ni ya uongo yaani ni vichekesho na sina cha kuongea zaidi,” alisema Asika.

Facebook Comments