Loading...
Home Makala MASTAA WALIOTIBUANA NA WAZAZI WAO

MASTAA WALIOTIBUANA NA WAZAZI WAO

254
SHARE

KUNA usemi usemao ‘uchungu wa mwana aujuaye mzazi’, ukiwa na maana kuwa mama ndiye mwenye uchungu zaidi na mtoto wake.  Ni kutokana na usemi huo, wapo wazazi ambao wamekuwa si wavumilivu na kushindwa kuzuia hisia zao pale watoto wao wanapokuwa wanafanya vitu visivyoeleweka katika jamii.

Lakini, wapo ambao wamekuwa wazito kuweka wazi hisia zao. Si kwa sababu hawawapendi watoto wao au hawana uchungu nao, bali wakifanya hivyo ili kujisitiri dhidi ya mashambulizi kutoka upande wa pili. Katika makala haya, yanaweka wazi top 5 ya mastaa ambao waliingia kwenye migogoro na wazazi wao baada ya kuwaendea kinyume, pindi tu walipopata umaarufu. Hivyo, kama mzazi kusimama kwenye msingi wake inakuwa ni kosa kwa upande wao.

WEMA

Mara nyingi staa huyu mwenye jina kubwa, huwa anaingia kwenye mgogoro na mama yake mzazi; Mariam Sepetu kutokana na vitu anavyofanya mwanaye ambavyo hapendezwi navyo kabisa. Kuna kipindi walishawahi kukaa bila hata salamu. Mzazi anafanya hivyo, kama njia sahihi ya kumuonya na kumkanya mtoto wake na mwisho wa siku utawaona pamoja wakiwa wapo kwenye harakati zao za kila siku kama mtoto na mama yake. “Nampenda sana mwanangu, hivyo inapotokea kutokuwa na maelewano baina yangu na yeye, ni marekebisho tu ya mama na mtoto na si kitu kingine,” aliwahi kusema mama huyo

MUNA

Staa huyu, tatizo la kutokuwa na maelewano na mama yake mzazi linaonekana ni pana, mpaka kufikia hatua Muna kumkana na kudai kuwa si mama yake mzazi na kusema kwamba mama yake alishafariki dunia zamani. Lakini kwa upande wa pili kwa watu wanaomfahamu Muna na mama yake, wanadaia msanii huyo kalewa umaarufu mpaka kusababisha kuona mama yake hana tena thamani kwake. Hivyo, kufikia mpaka hatua ya kupelekana polisi.

UWOYA

Staa huyo mwenye mvuto kwenye familia, kwao wamebahatika kuzaliwa wawili tu; akiwa yeye na mdogo wake wa kiume, Babuu. Amekuwa akiingia mgogoro wa mara kwa mara na mama yake mzazi, tangu kipindi akiwa na mumewe; marehemu Hamad Ndikumana, ikiwa ni moja ya kumsihi atulie kwenye ndoa yake. Staa huyo hakuwa vizuri tena na mama yake huyo baada ya kufunga ndoa na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ akiamini yeye alikuwa mke wa mtu, hakupaswa kufanya hivyo na yote ilikuwa ni kumnyoosha mtoto wake huyo awe kwenye mstari mzuri.

QUEEN DARLEEN & DIAMOND

Wawili hawa ambao wanafanya Muziki wa Bongo Fleva, ni ndugu kwa kuchangia baba, wamekuwa karibu na hata kusaidiana katika kazi za muziki na maswala ya kifamilia pia.

Ukiachana na hilo, kwa kipindi kirefu wanadaiwa kuwa na mahusiano ambayo si mazuri kwa baba yao, Abdul Jumaa na hata kufikia kipindi mzee huyo kuwatamkia maneno ambayo si mazuri. Mzee Abdul amekuwa akidai kutopewa heshima kama mzazi na pia kutothaminiwa ikiwa ni pamoja na kutengwa.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Facebook Comments