Loading...
Home Habari BREAKING: ALIYENUSURIKA AELEZA A-Z “DEREVA ALIKUWA BIZE NA SIMU” – VIDEO

BREAKING: ALIYENUSURIKA AELEZA A-Z “DEREVA ALIKUWA BIZE NA SIMU” – VIDEO

435
SHARE

MMOJA wa watu walionusurika kwenye ajali ya kuzama kwa MV Nyerere, Mchori Bulola amesema chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mzigo mkubwa ambao kivuko hicho kilikuwa imebeba.

Bulola amedai kutokana na hali hiyo, abiria walimueleza kapteni aliyekuwa akiendesha kivuko hicho lakini hakujali hivyo safari ilianza.

Lakini wakiwa njiani, amedai kapteni huyo alikuwa akizungumza kwenye simu, alishoshtuka alikuta tayari kivuko kimeshahama kwenye uelekeo wa daraja hivyo alilazimika kukata kona haraka jambo ambalo lilisababisha mzigo kuegemea upande mmoja.

 

Kutokana na hali hiyo kivuko hicho kilizama majini na kusababisha ajali iliyoua takribani watu 160. Aidha miili zaidi ya 21 imeopolewa kwa leo Jumamosi.

Facebook Comments