Loading...
Home Habari MJUE MBUZI DAMASI ANAYEFANYA ULINZI, ANAKULA MAANDAZI, NYAMA, WALI- VIDEO

MJUE MBUZI DAMASI ANAYEFANYA ULINZI, ANAKULA MAANDAZI, NYAMA, WALI- VIDEO

626
SHARE

KAMA ulikuwa hufahamu chukua hii! Mzee Antony Mwandulami mkazi wa Mkoa wa Njombe Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania anafuga mbuzi kama mlinzi wake.

Mzee Mwandulami anasema mbuzi huyo ambaye amefanya kazi kwake kwa miaka 19 sasa humpa taarifa juu ya kila mtu mbaya anayetaka kuja kwake na kumdhuru na ameweza kumnusuru dhidi ya majanga mbalimbali.

”Huyu anaitwa Damas kazi yake ni kufanya ulinzi hapa nyumbani yani kama kunatatizo yeye ndiyo anayejua, kwa mfano wanaingia majambazi,” amesema Mzee Antony.

Mwandulami ameongeza ”Akipata taarifa huko ananijulisha kama kunatatizo huwa ananijulisha, anakula maandazi na chai, wali na nyama za kuku na mbuzi anakula na kwa mfano mchana akitaka kunywa maji anakwenda kufungua bomba na kunywa maji mwenyewe na anafunga na kuondoka. Kama kunamtu anataka kuniteka ama kuvamiwa na majambazi natumia fimbo hii ila mbuzi ndiye anayenipa taarifa.”

Damas amekuwa akifanya kazi ya ulinzi usiku na mchana kwa zaidi ya miaka 19 sasa huku chakula chake kikuu kikiwa ni maandazi, nyama za kuku, mbuzi na wali.

Facebook Comments