Loading...
Home Habari Video: Marais 5 wanaolindwa zaidi duniani

Video: Marais 5 wanaolindwa zaidi duniani

581
SHARE

Katika taifa lolote lile dunia, Rais (Mfalme/Malkia) ndiye kiongozi wa juu zaidi na hivyo nguvu kubwa huelekezwa katika kuhakikisha usalama wake kwani endapo tatizo lolote litampata, mfano kuuawa, ajali, basi taifa husika litakuwa katika kipindi cha mpito hadi hapo atakapopatikana kiongozi mwingine wa kuchukua nafasi yake.

Kutokana na umuhimu wa juu wa viongozi hawa, sababu ya nafasi wanazoshikilia, mara nyingi ulinzi wao huimarishwa sana, hasa pale wanapokuwa katika maeneo ambayo ni hatarishi mfano kwenye mikusanyiko ya watu, barabarani.

Lakini, licha ya kuwa viongozi wote hawa ni muhimu kwa kila taifa husika, ulinzi wao hutofautiana. Kuna baadhi ya marais ambao hulindwa zaidi, na wengine huwa na ulinzi lakini sio wa hali ya juu kama wa mataifa mengine.

Ulinzi wa Rais wa taifa husika huimarishwa zaidi endapo kutakuwa na vitisho kutoka kwa vikundi vya kugaidi au kama taifa linahofia kuwepo wa vitisho kutoka kwa mataifa mengine.

Kati ya viongozi wote dunia, viongozi watano wanaolindwa zaidi ni;-

  1. Narendra Modi – Waziri Mkuu wa India
  2. Kim Jong-un – Rais wa Korea Kaskazini
  3. Vladimir Putin – Rais wa Urusi
  4. Elizabeth II – Malkini wa Uingereza na nchini nyingine za Jumuiya ya Mdola.
  5. Donald Trump – Rais wa Marekani

Hapa chini ni video ikionesha namna ulinzi wao unavyokuwa. Tazama kisha washirikishe na wengine;

Facebook Comments