Loading...
Home Michezo MICHEZO Yanga wameanza Ligi, Makambo swahiba wa nyavu

MICHEZO Yanga wameanza Ligi, Makambo swahiba wa nyavu

574
SHARE

Baada ya Bingwa mtetezi kucheza game yake ya ufunguzi ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu 2018/19 Simba SC na kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, leo watani zao wa jadi Yanga waliingia uwanja wa Taifa kuanza Ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Yanga leo wamefanikiwa kuanza Ligi vizuri baada ya kufanikiwa kuzichukua point tatu kwa kuifunga Mtibwa Sugar kwa magoli 2-1, magoli ya Yanga yakifungwa na Herieter Makambo dakika ya 31 na Kelvin Yondani kwa mkwaju wa penati dakika ya 40 wakati goli pekee la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 72.

Ushindi huo sasa Yanga utawaweka pazuri katika mbio za kurudisha taji la Ligi Kuu ambalo walinyang’anywa na watani zao Simba SC msimu uliopita, hadi game inamalizika Mtibwa Sugar walikuwa wakiutawala mchezo zaidi ya Yanga kwa asilimia 54 kwa 46.

Facebook Comments