Loading...
Home Michezo Hivi ndivyo Simba SC walivyoanza kutetea Ubingwa wao wa Ligi Kuu

Hivi ndivyo Simba SC walivyoanza kutetea Ubingwa wao wa Ligi Kuu

714
SHARE

Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeanza leo Jumatano ya August 22 2018 kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, Mabingwa watetezi Simba SC wao walikuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuikabili Tanzania Prisons.

Simba SC ambayo kwa sasa inatajwa kuwa ndio timu ambayo iko vizuri kila idara kuanzia kiuchumi hadi safu ya ujsajili, leo imefanikiwa kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0, kiasi cha kwamba mashabiki wa wapinzani wao wameanza kuwabeza kuwa kambi ya Uturuki haijawasaidia kitu.

Goli pekee la Simba SC lilifungwa na mshambuliaji wao mpya aliyena msimu wa kwanza Tanzania Meddie Kagere dakika ya 2 ya mchezo, baada ya mchezo huo Yanga kesho wataanza Ligi kwa kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Matokeo ya game za VPL zilizochezwa leo Jumatano ya AUgust 22 2018.

Facebook Comments