Loading...
Home Michezo Simba yashinda ngao ya jamii na kuweka historia

Simba yashinda ngao ya jamii na kuweka historia

611
SHARE

Hatimaye klabu ya Simba imefanikiwa kushinda kombe la kwanza la msimu huu baada ya kuichapa Mtibwa Sugar katika mchezo wa ngao ya jamii kuashiria ufunguzi wa pazia la ligi kuu Tanzania bara.

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao katika mchezo wao wa ngao ya jamii

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, umeshuhudiwa Simba wakiichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1, mabao ya Simba yakifungwa na mshambuliaji raia wa Rwanda, Meddie Kagere katika dakika ya 29 na Hassan Dilunga katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza huku bao pekee la Mtibwa Sugar likifungwa na Kevin Kongwe Sabato katika dakika ya 33 ya mchezo.

Kwa ushindi huo, sasa Simba inaweka historia ya kushinda kombe hilo mara nyingi zaidi kuliko klabu nyingine yoyote, ikiwa imeshinda mara sita ikifuataiwa na Yanga ambayo imeshinda mara tano. Mtibwa Sugar yenyewe ikiwa imeshinda mara moja pekee.

Ufunguzi rasmi wa ligi kuu Tanzania bara utafanyika Jumatano ijayo, 22 Agosti kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofautitofauti.

Michezo ya ufunguzi itakayochezwa ni pamoja na Simba ikiwakaribisha Tanzania Prizons ya Mbeya, Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji dhidi ya Ndanda Fc, Alliance Fc dhidi ya Mbao Fc, Coastal Union dhidi ya Lipuli Fc, Singida United watamenyana na Biashara United na Kagera Sugar wakiwaalika Mwadui Fc.

Agosti 23 ratiba ya ligi hiyo itaendelea kwa michezo minne, Stand United wakiwaalika African Lyon, JKT Tanzania dhidi ya KMC, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar na Azam FC dhidi ya Mbeya City

Facebook Comments