Loading...
Home Michezo Mmemmiss Wenger eeh? kwa mara ya kwanza tangu 1992 Arsenal wakutwa na...

Mmemmiss Wenger eeh? kwa mara ya kwanza tangu 1992 Arsenal wakutwa na janga hili

173
SHARE

Assist ya Marco Alonso dakika ya 9 ilizaa bao lililowekwa kimiani na Pedro, na hii inamfanya Alonso kuhusika katika mabao 19 tangu aanze kuichezea Chelsea(magoli 13, assists 6).

 

Cesar Azpilicueta naye alitoa assist kwa bao la pili la Alvaro Morata, na sasa assists zote 7 za Azpilicueta tangu msimu uliopita zilizaa mabao ya Morata na sasa anakuwa mchezaji aliyetoa assists nyingi kwa mwenzake katika EPL tangu msimu uliopita.

 

Henrikh Mkhitaryan aliifungia Arsenal bao la kwanza na sasa anakuwa amehusika katika mabao 8 katila mechi 13 tu Arsenal wakati akiwa United alihusika na mabao 7 katika mechi 25 alizoichezea United.

 

Alex Iwobi aliisawazishia Arsenal dakika ya 41 na kuufanya mchezo kwenda halftime kwa sare ya 2-2, idadi ya mabao Arsenal waliyofunga leo kipindi cha kwanza ni mengi kuliko waliyoifunga Chelsea katika mechi 6 zilizopita Stamford Bridge.

 

Marcos Alonso alifunga bao la 3 kwa upande wa Chelsea ambalo linamfanya kuhusika katika mabao 20 tangu ajiunge na Chelsea, magoli 14 na assists 6.

 

Goli la Alonso lilitokana na assist ya Eden Hazard na sasa ni Frank Lampard 90, Didier Drogba 55 na Gianfranco Zola 42 ndio wachezaji pekee wenye assists nyingi katika historia ya Chelsea kuliko Eden Hazard 41.

 

Mara ya mwisho kwa Arsenal kupoteza michezo miwili ya mwanzo ya EPL ilikuwa msimu 1992/193 chini ya George Graham ambapo walifungwa mechi ya kwanza na Norwich kisha wakapigwa na Blackburn na hii ni mara ya pili tangu mwaka huo wanapoteza mara mbili mfululizo.

Facebook Comments