Loading...
Home Michezo AHMED MUSA AFUFUA MATUMAINI YA NIGERIA KOMBE LA DUNIA

AHMED MUSA AFUFUA MATUMAINI YA NIGERIA KOMBE LA DUNIA

343
SHARE

Timu ya taifa ya Nigeria baada ya kupokea kipigo chake cha kwanza katika mchezo wao dhidi ya Croatia kwa magoli 2-0, leo ilicheza mchezo wake wa pili wa World Cup 2018 dhidi ya Iceland.

Ahmed Musa

Nigeria leo dhidi ya Iceland wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, shukrani za kipekee kwa Ahmed Musa aliyefunga magoli yote mawili dakika ya 48 na 74 kutokana na kuwa na utulivu katika eneo la hatari na kuzitumia nafasi zote mbili kwa ufasaha.

Ushindi huo sasa unawaweka pazuri Nigeria na kuwapa imani Argentina kuwa wanaweza kufuzu hatua ya 16 bora kwani kufuzu kwa Argentina na Nigeria kutatokana na timu zote mbili kupata ushindi zitakapo kutana June 26 ila Nigeria hata sare inamvusha hatua inayofuata.

Croatia tayari amefuzu hatua ya 16 kutokana na kupata ushindi mechi mbili na kuwa na point 6, wakati Nigeria wao wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point tatu, Iceland nafasi ya tatu kwa kuwa na point moja sawa na Argentina walio nafasi ya nne kwa kutofautiana magoli ya kufungwa.

Facebook Comments