Loading...
Home Michezo Urusi Yaanza Vyema Kombe La Dunia….Yaitandika Saudi Arabia Bao 5-0

Urusi Yaanza Vyema Kombe La Dunia….Yaitandika Saudi Arabia Bao 5-0

316
SHARE

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Luzhniki kwa wenyeji Urusi kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 dhidi ya Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia.

Mechi hiyo ya aina yake imeshuhudiwa bao la kwanza likiwekwa kimiani mnamo dakika ya 12 na Ganzizky ambalo limeandika rekodi ya kuwa bao la kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu.

Mabao mengine yametiwa kimiani na Cheryshev (43′ minutes, 90’+1), Dzyuba (71′ ) na Golovin (90’+4).

Baada ya wenyeji kuanza vizuri, mechi zingine za kesho zitakuwa ni Iran itakayowakaribisha Morocco na vilevile Ureno itakuwa inacheza dhidi ya Spain.

Facebook Comments