Loading...
Home Habari Askofu Wa KKKT Dayosisi Ya Kuini Mashariki Awaomba Radhi Waumini Na Maaskofu.

Askofu Wa KKKT Dayosisi Ya Kuini Mashariki Awaomba Radhi Waumini Na Maaskofu.

472
SHARE

Askofu Mbedule ameomba radhi leo Aprili 29, 2018 wakati wa Ibada ya iliyofanyika kanisa la Mtwara Mjini, amesema licha ya salamu hizo kutokusomwa, anaunga nazo na yupo pamoja na maaskofu wenzake.

Akisoma barua ambayo ameituma kwa Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo na maaskofu wote wa kanisa hilo, Askofu Mbedule amesema baraka za mababa maaskofu zilishindwa kusomwa kwa sababu zilizojitokeza wakati huo.

“Kwa njia ya barua hii, kwanza napenda kuwaombeni radhi kwa kuwakosesha baraka za mababa maaskofu,” amesema Askofu Mbedule. Amesema yeye alishiriki kuuandaa na kutia saini na yupo pamoja na maaskofu wenzake.

Facebook Comments