Loading...
Home Burudani na Wasanii Alikiba Agoma Kumualika Diamond Kwenye Sherehe ya Harusi Yake Inayofanyika Dar Leo

Alikiba Agoma Kumualika Diamond Kwenye Sherehe ya Harusi Yake Inayofanyika Dar Leo

4034
SHARE

Licha ya habari kusema kuwa Diamond yupo tayari kuhudhuria sherehe ya harusi ya Alikiba Jioni Ya leo hii, lakini upande wa Diamond umesema hajaalikwa. Chanzo kilicho karibu na Alikiba kimeiambia AVMEDIA.

“Kiba anaonekana bado hayuko poa na Diamond, kamfanyia mwenzake jambo la kushangaza sana maana huwezi amini hadi dakika hii hajamualika kwenye sherehe yake ya harusi, yaani inaonekana Kiba hayuko tayari kushirikiana na mwenzake maana mara nyingi amekuwa akijishusha lakini hampi ushirikiano,”

Nae Aidan Seif ambaye ni meneja wa Alikiba alipoulizwa na AVMEDIA kuhusu issue hiyo amesema.

“Hadi sasa hatujamualika na kwa kweli sijajua kama tutamualika,” .

Facebook Comments