Loading...
Home Habari Top 10 ya shule za gharama kubwa zaidi nchini Tanzania

Top 10 ya shule za gharama kubwa zaidi nchini Tanzania

8791
SHARE

Shule  za Msingi na Sekondari zinaweza kuwa elimu ya gharama kubwa katika baadhi ya nchi hapa chini, ni baadhi ya Shule zilozopo Tanzania ambazo hutoza gharama kubwa za ada kwa mwaka ikiwa ni ya ada ya masomo.

10. Morogoro International School (MIS)
Katika Shule ya MIS ada yake kwa mwanafunzi ni kati ya Sh 4.4 Milioni  kwa shule ya Chekechea na Sh 17 milioni kwa elimu ya  Sekondari. Shule hii ni ya gharama kubwa zaidi katika eneo la mkoa wa Morogoro. Shule inatumia mtaala wa Cambridge.

9. International School of Moshi (ISM)
ISM ni shule ghali zaidi katika eneo la Moshi. Ada ya kila mwanafunzi kwa mwaka ni kati ya Sh 14.5 Milion kwa elimu ya msingi na Sh 17.2 Milioni  kwa elimu ya Sekondari. Shule inatumia mtaala wa IB.

8. Aga Khan Shule ya Msingi na Sekondari

Aga Khan ipo nafasi ya nane kwa Shule za gharama kubwa Tanzania. Ipo katika eneo la Dar es salaam. Mwanafunzi wa ngazi ya msingi,  kila mwaka ada ni  kati ya Sh 7.2 Milioni na Sh 20.4 Milioni kwa ngazi ya sekondari. Aga Khan inatumia mtaala wa IB.

7. Hope of Peace Academy (HOPAC)
Hopac ni Shule ya kikristo ya Kimataifa inayopatikana Dar es salaam, na kila mwaka ada ya shule ya msingi huanzia Sh 15.5 Milioni hadi kufikia Sh 21.Milioni kwa ngazi ya Sekondari. HOPAC inatumia mtaala wa Cambridge.

6. Kennedy House Schools
KHS ni kundi la shule zilizopo sehemu mbalimbali duniani kote. Tanzania wana shule yao inayopatikana Arusha ambapo hutoa elimu kwa ngazi ya Awali na Msingi. Ada zao ni kati ya Sh 7.8 Milioni kwa elimu ya awali(pre-primary) hadi kufikia Sh 22.4 Milioni kwa elimu ya Msingi. Inatumia mtaala wa Cambridge.

5. St Constantine International School
St Constantine ni shule ya Kimataifa ya bweni na kutwa. Ni ya pili kwa shule za gharama kubwa kwa mkoa wa Arusha. Kila mwaka ada ya elimu ya msingi ni kuanzia Sh 7.5Milioni  na Sh 22.8Milioni kwa ngazi ya Sekondari. Inatumia mtaala wa Cambridge.

4. Iringa International School (IIS)
IIS ni shule ya gharama kubwa zaidi katika Shule zote za mkoa wa Iringa. Imepitisha na kufundisha mitaala miwili ya IB na Cambridge . Ili kupata elimu yao ya msingi kila mwaka utatozwa ada ya kati ya Sh16.7 Milioni na kutoa Sh 27.4Milioni kwa elimu ya Sekondari.

3. Dar es Salaam International Academy (DIA)
DIA ni ya tatu yenye gharama kubwa kwa Shule zilizopo nchini Tanzania. Ipo katika eneo la Dar es Salaam na hutoa elimu yake kupitia mtaala wa IB. Ada yake ya kila mwaka ni kati ya Sh 24.3 milioni na elimu ya sekondari utaipata kwa Sh40 milioni.

2. Braeburn International School
Braeburn ni shule ya kimataifa ya kutwa na bweni. Hutoa elimu kupitia mtaala wa IB. Inapatikana mkoa wa Arusha na Dar es Salaam. Kupata elimu yake ya msingi, kila mwaka utatozwa ada ya kati ya Sh 20.3 Milioni na utalazimika kulipa Sh 42.6 Milioni kwa elimu ya Sekondari.

1. Interntional School of Tanganyika (IST)
IST ndiyo shule inayotoza gharama zaidi kuliko shule zote nchini Tanzania. Inapatikana katika mkoa wa Dar es Salaam na hutumia mtaala wa IB. Ili kupata elimu yake ya msingi, kila mwaka itakubidi ulipe ada inayofikia Sh 33.3Milioni na Sh 65.5Milioni ikiwa ni ada kwa elimu ya Sekondari.

Facebook Comments