Loading...
Home Habari PICHA: Tundu Lissu Ameweza Kukaa Mwenyewe

PICHA: Tundu Lissu Ameweza Kukaa Mwenyewe

499
SHARE

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amekaa mwenyewe pasipo msaada wa madaktari katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, anakotibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, Area D, Dodoma huku hali yake ikizidi kuimarika kila kukicha.

Desemba 26, mbunge huyo alisimama kwa mara ya kwanza na kuanza rasmi kufanya mazoezi ya viungo katika Hospitali hiyo kwa msaada wa madaktari. Lissu anaendelea na mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze kutembea.

Akielezea hali yake, Mhe. Tundu Lissu amesema kwa sasa anauwezo wa kukaa bila kuegemea kwenye kitu chochote, hali ambayo awali alikuwa anashindwa kufanya hivyo.

“Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu. Sasa ninaweza kukaa bila ya kuegemea kitu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, hivi karibuni alisema bado ana risasi moja mwilini mwake ambayo haijatolewa.

Facebook Comments