Loading...
Home Michezo Kwa kipigo cha Barcelona , Real Madrid ndio basi tena

Kwa kipigo cha Barcelona , Real Madrid ndio basi tena

350
SHARE

Baada ya kuusubiri kwa hamu mchezo wa El Clasico wa Real Madrid dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu uliyochezwa jioni ya December 23 2017, hatimae time ikafika na tukashuhudia mchezo huo.

Real Madrid wakiwa katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu wakutana na kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya FC Barcelona, licha ya Real Madrid mwanzoni kuutawala mchezo, magoli ya Barcelona yalifungwa na Luis Suarez dakika ya 54, Lionel Messi kwa penati dakika ya 64 na Aleix Vidal dakika ya 93.

Baada ya kipigo hiko wengi wameanza kusema Real Madrid itakuwa ngumu katika mbio za kuwania Ubingwa wa LaLiga kutokana hadi sasa watakuwa wameachwa na Barcelona wanaoongoza Ligi kwa tofauti ya point 14 Real Madrid wakiwa na mchezo wa kiporo mkononi.

Msimamo wa LaLiga baada ya game ya El Clasico

Facebook Comments