Loading...
Home Michezo MESSI, SUAREZ WAIADHIBU MADRID, BARCELONA IKISHINDA 3-0 UGENINI SANTIAGO BERNABEU

MESSI, SUAREZ WAIADHIBU MADRID, BARCELONA IKISHINDA 3-0 UGENINI SANTIAGO BERNABEU

412
SHARE
FC Barcelona imezidi kujichimbia kileleni mwa La Liga baada ya kuitwanga Real Madrid kwa mabao 3-0 katika El Clasico mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Mechi hiyo ilikuwa tamu na ya kuvutia na hadi mapumiziko hakukuwa na mbabe aliyegusa nyavu za mwenzake.
Kipindi cha pili kilikuwa kichungu kwa Madrid ambayo ilikubali mabao mawili ya Luis Suarez na Lionel Messi aliyefunga kwa mkwaju wa penalti huku Madrid ikicheza pungufu baada yabeki wake wa kulia, Dani Carvajal kulambwa kadi nyekundu baada ya kuunawa mpira makusudi akiuzuia usitinge wavuni.

 

Alex Vidal aliyeingia dakika tatu kabla mpira kwisha, alifumga bao la tatu katika dakika ya 90 kwa mkwaju mkali kabisa, kipa alijaribu kudaka lakini ukamshinda.

 

Madrid walipata zaidi ya nafasi tatu za kufunga katika kipindi cha kwanza, lakini mabingwa hao wa dunia mara mbili mfululizo, walishindwa kufunga kupitia Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Facebook Comments